FidStyle Friday bado iko Rap City. Wiki hii Mwanza inawakilishwa na Mecco South: Kad Go, Malle, Roland na Biznea!
Ukiacha kuchana, wanatupa undani wa kitabu “Chuo Kikuu Cha Hip Hop” kilichoandikwa na Malle. Kitabu hiki kinajadili sanaa na utamaduni wa Hip Hop, kikitupa hoja chanya [zaidi] kulinganisha na jinsi utamaduni huu unavyochukuliwa na wengi au wenye fikra tofauti.
Baada ya hapo kila mmoja anaonesha uwezo wake akitumia midundo ya D Classics na J Ryder. Mtoto wa Mkulima anaulizwa, “Vipi? Mbona mizengo inapinda?” Wengine “… wanakula bila kunawa, walaji wakiwa wengi.” Kad Go naye anahoji mambo anayoyaona kwenye jamii: “… Vijana wameshiba uwoga, mitaa imeshiba soga, tangu jana tunajengwa kuwa taifa la mazoba!”
Nyongeza kwa wanaotumia mtandao:
Kurasa muhimu kuhusu Mecco South: